Gor Mahia imehifadhi taji la SportPesa Super Cup kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuwalaza mabingwa wa Tanzania Bara Simba mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa katika uwanja wa Afraha.
Mabao ya Meddy Kagere na Jack Tuyisenge yalitosha kuipa Gor Mahia ushindi muhimu unaowapeleka Uingereza kucheza na Everton pamoja na kushinda zawadi nyingine ya mashindano hayo Dola 30,000.
Simba ilipata wakati mgumu kwenda na kasi ya wapinzani wao waliokuwa wakicheza mpira wa kuzuia na kushambulia kwa pamoja 'toto Football'.
Kumekuwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa mashabiki baada ya uongozi wa Simba kutowajumuisha baadhi ya wachezaji muhimu katika kikosi kilichokwenda Kenya.
Wengi wanaamini kukosekana kwa washambuliaji tegemeo Emanuel Okwi na nahodha John Bocco kumepelekea Simba kutofunga hata bao moja la ndani ya mchezo.
Ushindi wa michezo iliyopita ulipatikana kwa mikwaju ya penati.
Kaimu Kocha wa Simba Masudi Djuma amesema walifanya makosa ambayo yalipelekea kufungwa mabao hayo mawili.
Amesema wamekubali matokeo hayo na wanarudi kujipanga upya kwa ajili ya mashindano ya msimu ujao.

ADVERTISE HERE