Singida United imefanikiwa kutwaa nafasi ya tatu ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Kakamega HomeBoyz kwa mikwaju ya penati 4-1 kufuatia sare ya bao 1-1.
Mchezo huo umepigwa mapema saa sita mchana kwenye dimba la Afraha ili kupisha mchezo wa fainali unaotarajiwa kuanza saa tisa.
Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba watachuana na Mabingwa wa Kenya Gor Mahia kwenye mchezo huo wa fainali unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka Afrika Mashariki.
Bingwa wa michuano hiyo atajinyakulia kitita cha Dola 30,000 pamoja na kupata tiketi ya kwenda nchini Uingereza kucheza na Everton.

ADVERTISE HERE