Wanaowania tuzo ya mchezaji bora VPL wachujwa na kubaki 15

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Jun 2018
Wanaowania tuzo ya mchezaji bora VPL wachujwa na kubaki 15
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msimu wa mwaka 2017/2018, ambayo sherehe zake zimepangwa kufanyika Juni 23 mwaka huu.

Wachezaji hao 15 ni miongoni mwa 30 waliotangazwa awali wiki mbili zilizopita kuwania tuzo hizo, ambapo watachujwa kulingana na takwimu mbalimbali za ligi hiyo na kubakia watatu.

Majina ya wachezaji hao watatu yanatarajiwa kutangazwa wiki ijayo, ambapo pamoja na takwimu ambazo Kamati ya Tuzo inazo, pia itahusisha upigaji wa kura kutoka kwa wahariri wa habari za michezo, manahodha wa timu za Ligi Kuu pamoja na makocha wa timu za Ligi Kuu.

Wachezaji hao 15 na majina ya timu zao katika mabano ni Obrey Chirwa, Papy Tshishimbi na Kelvin Yondani (Yanga), Shafiq Batambuze, Mudathir Yahya na Tafadzwa Kutinyu (Singida United).

Wengine ni Adam Salamba (Lipuli), Habibu Kyombo (Mbao), John Bocco, Emmanuel Okwi, Shiza Kichuya na Erasto Nyoni (Simba), Marcel Kaheza (Majimaji), Yahya Zayd (Azam) na Hassan Dilunga (Mtibwa).

Licha ya Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL, pia siku hiyo katika sherehe zitakazofanyika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam kutatolewa tuzo mbalimbali ikiwemo ya Bingwa wa VPL, Mshindi wa Pili, Mshindi wa Tatu, Mshindi wa Nne na Mfungaji Bora.

Tuzo nyingine ni Timu yenye Nidhamu Bora, Mchezaji Bora wa Ligi ya Vijana (Tuzo ya Ismail Khalfan), Mchezaji Bora Chipukizi, Mwamuzi Msaidizi Bora, Mwamuzi Bora,Kipa Bora, Kocha Bora, Goli Bora, Kikosi Bora cha Msimu na Mchezaji wa Heshima.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
2h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
20h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’