Mwakyembe 'aifagilia' Simba kutinga fainali SporPesa Super Cup

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Jun 2018
Mwakyembe 'aifagilia' Simba kutinga fainali SporPesa Super Cup
Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe ameipongeza klabu ya Simba kwa kufanikiwa kutinga fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup inayofanyika Nakuru, Kenya.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo, Dk Mwakyembe amesema mafanikio hayo huko Kenya yanadhihirisha Simba haikubahatisha kutwaa ubingwa wa VPL msimu huu.

"Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Simba kwa kufanikiwa kutinga fainali ya SportPesa Super Kenya, wamethibitisha kuwa walichukua ubingwa wa ligi si kwa kubahatisha kwa soka la kiwango" amesema.

Dk Mwakyembe amezishauri timu nyingine za Tanzania kufanya uwekezaji mkubwa kama zilivyofanya klabu za Simba na Singida United ili kupata mafanikio.

Simba itachuana na Gor Mahia kwenye mchezo wa fainali utakaopigwa katika uwanja wa Afraha keshokutwa Jumapili, Juni 10 ukitarajiwa kuanza saa tisa kamili Alasiri.

Simba ilitinga fainali baada ya kuziondoa kwa mikwaju ya penati timu za K. Sharks na Kakamega HomeBoyz zote kutoka nchini Kenya.

Gor Mahia nayo ilitinga fainali kwa kuzifunga JKU na Singida United zote kutoka Tanzania.

Singida United na KK HomeBoyz zitacheza kusaka mshindi wa tatu.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
29m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’