Fainali ni Simba dhidi ya Gor Mahia

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Jun 2018
Fainali ni Simba dhidi ya Gor Mahia
Mchezo wa fainali ya michuano ya SportPesa Super utawakutanisha mabingwa wa Tanzania Bara, Simba dhidi ya Mabingwa wenzao wa Kenya, Gor Mahia.

Gor Mahia imeifuata Simba fainali baada ya kuilaza Singida United mabao 2-0 kwenye mchezo wa pili wa nusu fainali.

Meddy Kagere, mshambuliaji hatari wa timu hiyo ndiye aliyeifunga mabao yote mawili.

Kagere ndiye kinara wa mabao katika michuano hiyo akiwa amefunga mabao matatu.

Mapema kabla ya mchezo huo, Simba ilitinga fainali kwa kuiondosha Kakamega HomeBoyz kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya timu hizo kutoka suluhu katika muda wa dakika 90.

Mchezo wa fainali utapigwa Jumapili, Juni 10, 2018 katika uwanja wa Afraha.

Bingwa wa michuano hiyo atajinyakulia kitita cha Dola 30,000 pamoja na kupata tiketi ya kusafiri nchini Uingereza kwenda kuchuana na Everton katika dimba la Goodison Park.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’