Mabingwa wa Tanzania Bara Simba wametinga fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya suluhu ya bila kufungana dhidi ya Kakamega HomeBoyz.
Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Afraha, Nakuru Kenya uliishuhudia Simba ikitawala kwa muda mwingi na kufanya mashambulizi kadhaa langoni kwa Kakamega lakini ilishindwa kutumbukiza mpira nyavuni.
Simba ilifanikiwa kufunga mikwaju yake yote mitano ya penati iliyopigwa na Haruna Niyonzima, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Shiza Kichuya na Jonas Mkude.
Simba sasa inamsubiri mshindi kati ya Singida United dhidi ya Gor Mahia kwa ajili ya mchezo wa fainali utakaopigwa Jumapili, Juni 10 2018.

ADVERTISE HERE