Mlinda lango namba moja wa Simba Aishi Manula jana asubuhi alishindwa kufanya mazoezi kutokana na maumivu ya goti aliyopata kwenye mchezo dhidi ya K. Sharks juzi.
Manula aligongana na beki Paul Bukaba kupelekea kuumia goti la kulia.
Lakini aliweza kuendelea na mchezo na kuiwezesha Simba kutinga nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup inayoendelea Nakuru, Kenya.
Daktari wa Simba Yassin Gembe amesema anamatumaini makubwa kuwa Manula atakuwepo uwanjani kwenye mchezo ujao wa nusu fainali hapo kesho dhidi ya KK HomeBoyz.

ADVERTISE HERE