Kocha Msaidizi wa Simba Masudi Djuma amekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amejiuzulu nafasi yake.
Kocha huyo amesema hafahamu taarifa hizo zimetoka wapi lakini ukweli ni kwamba yeye hana mpango wa kuondoka Simba.
"Mimi nina mkataba na klabu ya Simba. Nimetoka nyumbani kuja kufanya kazi Simba. Sina mawazo ya kuondoka leo au kesho, labda wenyewe ndio waniondoe," amesema Djuma.
Djuma amekuwa akipigiwa chapuo akabidhiwe mikoba ya kocha Pierre Lechantre ambaye mkataba wake wa kuitumikia Simba unamalizika Juni 18, 2018.

ADVERTISE HERE