Salamba kuongezwa kikosi cha Simba Kenya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Jun 2018
Salamba kuongezwa kikosi cha Simba Kenya
Mshambuliaji mpya wa Simba Adam Salamba aliyesajiliwa kutoka klabu ya Lipuli FC leo anatarajiwa kusafiri kwenda nchini Kenya kuungana na kikosi cha Simba kilichotinga nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup.

Baada ya kufanikiwa kuiondoa kwa mikwaju ya penati, K Sharks jana, keshokutwa Simba itacheza na Kakamega HomeBoyz katika mchezo wa nusu fainali.

Katika mchezo huo wa jana, Simba ilionyesha madhaifu makubwa kwenye safu yake ya ushambuliaji hivyo kupelekea mahitaji ya kuongezwa nguvu kwa wachezaji wazoefu.

Simba inawategemea washambuliaji wake wapya Mohammed Rashid na Marcel Kaheza wakisaidiana na Mohammed Ibrahim 'Mo'.

Hata hivyo washambuliaji hao wanahitaji muda zaidi kuweza kwendana na kasi ya Simba.

Washambuliaji tegemeo ya Simba, nahodha John Bocco na Emanuel Okwi hawakusafiri na Simba nchini Kenya, Bocco akidaiwa kuwa na matatizo ya kifamilia wakati Okwi akiwa ameruhusiwa kurejea Uganda kwa mapumziko.

Wachezaji wengine wa Simba ambao hawakusafiri ni pamoja na Asante Kwasi, James Kotei na Nicolas Gyan wote wakiwa wamepewa ruhusa ya kurejea kwao Ghana kwa mapumziko.

Mbali na Salamba, huenda nahodha Bocco naye akaungana na Simba nchini Kenya
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
12h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
15h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’