Ni dhahiri mashabiki wa Simba wamemchoka Kocha Mkuu wa timu hiyo Pierre Lechantre wakitaka uongozi wa timu hiyo umuondoe na mikoba yake akabidhiwe msaidizi wake Masudi Djuma.
Licha ya kuwa Simba imeshinda michezo mingi chini yake, mfumo wake umekuwa ukikosolewa na wengi.
Lechantre amekuwa akitumia mfumo wa kujihami zaidi unaoinyima Simba ushindi mnono tofauti na wakati timu hiyo ilivyokuwa chini ya Djuma.
Lechantre anakiongoza kikosi cha Simba kinachoshiriki mashindano ya SportPesa Super Cup ambapo leo imetinga nusu fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 3-2 dhidi ya K. Sharks.
Kiwango cha chini kilichoonyeshwa na Simba kwenye mchezo huo kimewakera zaidi mashabiki na kuutaka uongozi umuondoe kocha huyo.
Wakati anajiunga Simba, Lechantre alisaini mkataba wa miezi sita ambao unamalizika mwezi huu.
Bado hakuna uhakika kama Bosi wa Simba Mohammed Dewji ataidhinisha Mfaransa huo kuongezwa mkataba mwingine ikielezwa kuwa mshahara wake ni kikwazo.

ADVERTISE HERE