Simba ilihitaji kuibuka na ushindi kwa namna yoyote katika mchezo dhidi ya K. Sharks ili iweze kusonga mbele kwenye michuano ya SportPesa Super Cup.
Ushindi wa mikwaju ya penati 3-2 umetosha kuipeleka Simba nusu fainali na sasa itachuana na wababe wa Yanga, Kakamega HomeBoyz, Juni 07.
Baada ya timu mbili za Yanga na JKU kutolewa mapema, timu za Simba na Singida United ndizo zilizosalia kwenye mashindano hayo.
Kesho Jumanne Singida United itacheza na AFC Leopards kwenye mchezo wa robo fainali.
Tayari timu mbili za Kenya zimetinga nusu fainali hivyo imekuwa vizuri kwa Simba kutinga hatua hiyo huku tukiiombea Singida United ipate ushindi kesho ili Tanzania nayo iwe na timu mbili katika hatua hiyo pia.
Mwaka jana Gor Mahia ilitwaa taji hilo katika ardhi ya Tanzania, nasi mwaka huu ni lazima tutwae taji katika ardhi yao.
Simba imeanza taratibu michuano hiyo lakini bila shaka itaimarika zaidi kwenye mchezo ujao dhidi ya KK HomeBoyz kwa kuwa makocha wamebaini mapungufu na wataweza kuyafanyia kazi.

ADVERTISE HERE