Mkataba wa Lechantre Simba unaisha mwezi huu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
4 Jun 2018
Mkataba wa Lechantre Simba unaisha mwezi huu
Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre amesema, anashindwa kuendelea kupanga mipango mingi ndani ya Simba kwani mpaka sasa hafahamu hatma yake na huenda asiendelee tena kuinoa timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Lechantre amesema mpaka sasa hajafikia makubaliano yoyote ya mkataba mpya na Simba, lakini anamsikilizia mfadhali wa timu hiyo, Mohammed Dewji juu ya hatma yake hiyo.

“Nimegundua hapa watu wana matarajio makubwa sana. Niliposhinda mechi nyingi walikuwa kimya, tulipofungwa na kutoa sare watu wameumia sana. Nahitaji kupewa muda zaidi ili nitengeneze timu mpya,"amesema Lechantre.

“Mohammed Dewji ana programu nzuri hapa, inahitaji muda. Ni lazima tukubaliane kwamba kutengeneza timu ya kushinda taji la Afrika inahitajika muda zaidi, nitazungumza naye ili kuona tunafanya nini.

“Mpaka sasa sijafahamu hatma yangu, nashindwa kupangilia vitu vingi hivyo hata hao wachezaji wapya siwezi kusema nitawatumia vipi,” amesisitiza Mfaransa huyo aliyeomba kazi tena timu ya Taifa ya Cameroon.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
5h ago
READ MORE →
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
6h ago
READ MORE →
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
6h ago
READ MORE →
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
9h ago
READ MORE →
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
11h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE →
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE →