JKU yaungana na Yanga kurudi nyumbani mapema

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Jun 2018
JKU yaungana na Yanga kurudi nyumbani mapema
Mabingwa wa Zanzibar, JKU wameyaaga mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kulazwa mabao 3-0 na Gor Mahia katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Afraha, Nakuru Kenya.

Mabao ya George Odhiambo, Walusimbi na Meddy Kagere yaliihakikishia Gor Mahia, mabingwa watetezi wa michuano hiyo kutinga hatua ya nusu fainali na kuiacha JKU ikiungana na Yanga kurudi nyumbani mapema.

Mapema kabla ya mchezo huo, Yanga ililazwa mabao 3-1 na Kakamega HomeBoyz na kuwa ya kwanza kuyaaga mashindano hayo.

Ni Simba na Singida United pekee zilizobaki kwenye michuano hiyo inayoshirikisha timu nne kutoka Tanzania na nne kutoka Kenya.

Simba inacheza leo Jumatatu dhidi ya K. Sharks wakati Singida United itashuka dimbani Jumanne kucheza na AFC Leopards.

Bingwa wa michuano hiyo atajinyakulia kitita cha dola za Kimarekani 30,000 sambamba na kupata tiketi ya kwenda kucheza na Everton nchini Uingereza.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
5h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
9h ago
READ MORE β†’
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
9h ago
READ MORE β†’
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
12h ago
READ MORE β†’
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
12h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’