Djuma awaambia Yanga wajiandae kisaikolojia

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Oct 2017
Djuma awaambia Yanga wajiandae kisaikolojia
Kocha msaidizi wa Simba Masud Djuma, amesema kwa muda mfupi ambao amefanya kazi na timu hiyo amebaini namna walivyokuwa na kikosi bora ambacho hakina hofu ya kucheza na timu yoyote ikiwemo Yanga.

Djuma amesema pamoja na kuwa na siku chache Simba, lakini ameweza kuwafuatilia kwa umakini wapinzani wao Yanga na kujiridhishwa kuwa ni timu ya kawaida isiyotisha hata kidogo kuelekea kwenye pambano hilo linalovuta hisia za mashabiki wengi wa soka Tanzania.

"Tuna kikosi imara sioni sababu ya mashabiki wa Simba, kuwa na hofu kwasababu maandalizi tunayofanya ni mazuri na wachezaji wote wapo na kila mmoja wetu amepania kuhakikisha tunashinda mchezo huo muhimu," amesema Djuma.

Kocha huyo ambaye ataanza kuonekana kwenye benchi la Simba kwa mara ya kwanza katika mchezo huo amesema imani yake ataendelea kuwa na furaha hadi mwishoni mwa msimu huu kwa maana timu hiyo itaendelea kufanya vizuri na kushinda kila mechi iliyopo mbele yao na kutwaa ubingwa.

Kocha huyo wa zamani wa Rayon Sport anajua presha iliyopo wakati timu hizo zikipambana lakini haoni kama kutakuwa na tofauti kubwa ya matokeo ukilinganisha na mchezo uliopita wakati timu hizo zilipokutana.

"Nimeambia mara ya mwisho Yanga walifungwa mabao 2-1 na Simba tena wakiwa nusu hicho ndicho kitakachotokea Jumamosi sioni mabadiliko kwasababu Yanga bado ni timu dhaifu na ni timu ambayo inacheza kwakutegemea uwezo wa mchezaji mmoja mmoja.

Djuma ameupongeza uongozi wa Simba, kwa maandalizi mazuri kuelekea mchezo huo na amesema haoni sababu ya kushindwa kupata ushindi kutokana na mandhari nzuri waliyonayo huko Visiwani Zanzibar.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
9h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
10h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
13h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’