Mabao mawili muhimu ya ugenini yamepatikana Zambia Simba ikilazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi Power Dynamos
Ni katika mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Alikuwa Clatous Chama aliyewaadhibu ndugu zake kutoka Zambia akifunga mabao yote mawili huku bao la pili akilifunga dakika za lala Salama
Simba ilikuwa bora zaidi kwenye kipindi cha pili na pengine ilipaswa kumaliza mchezo huo hukohuko Zambia
Lakini sare ya ugenini bado ni matokeo mazuri kwani sasa Simba inahitaji ushindi au sare ya chini na mabao mawili Ili kutinga hatua ya makundi
Mchezo wa marudiano utapigwa wiki ijayo katika uwanja wa Azam Complex