Wakatamiwa wa Mtibwa Sugar wametwaa kombe la FA (ASFC) baada ya kuilaza Singida United mabao 3-2 kwenye mchezo wa fanali uliopigwa katika dimba la Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.
Mtibwa Sugar ilipata mabao yake kupitia kwa Salum Kihimbwa 22', Issa Rashid 37' na Ismail Mheja 90' wakati yale ya Singida United yalipachikwa na Salum Chukwu 43' na Tafadzwa Kutinyu 70'.

Mchezo huo ulikuwa na upinzani mkali kutoka kila upande, Singida United ikitawala kwa muda mwingi lakini Mtibwa Sugar ikiwa na madhara zaidi langoni kwa Singida United.
Mtibwa Sugar ilimaliza na wachezaji 10 uwanjani baada ya mfungaji wake wa bao la pili Issa Rashid 'Baba Ubaya' kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika dakika ya 78 kwa kuonyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumtolea lugha chafu mwamuzi.

Ushindi huo umeipa Mtibwa Sugar nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu ujao huku ikijinyakulia kitita cha Mil 50.
Mchezo huo pia umehitimisha vibaya msimu wa kocha wa Singida United Hans van Pluijm anayekwenda kujiunga na Azam FC.
Mtibwa Sugar sasa inaungana na mabingwa wa Tanzania Bara, Simba kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao.
Simba itashiriki michuano ya ligi ya mabingwa wakati Mtibwa Sugar itashiriki kombe la Shirikisho.

ADVERTISE HERE