Habari za uhakika ni kwamba uongozi wa Simba umekuwa kwenye mazungumzo na mshambuliaji anayemaliza mkataba katika klabu ya Yanga, Mzambia Obrey Chirwa.
Hata hivyo kuna taarifa kuwa klabu ya Ismailia ya Misri nayo imeingia kwenye vita ya kuwania sahihi ya Mzambia huyo aliyeifungia Yanga mabao 12 msimu uliomalizika.
Mkataba wa Chirwa na Yanga unamalizika mwishoni mwa mwezi huu na hakuna matumaini kwa Yanga kuweza kumbakisha mshambuliaji huyo kutokana na hali yao ya kiuchumi.
Juzi katika mahojiano yake na gazeti moja la kila siku, Chirwa alisema ana ofa za timu nyingi kutoka nje ya Tanzania hivyo atafanya maamuzi pindi mkataba wake utakapokuwa umemalizika.

ADVERTISE HERE