Mshambuliaji mpya wa Simba Mohammed Rashid aliyesajiliwa juzi kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Tanzania Prisons, amesema hajatua Simba 'kuuza sura'.
Rashid aliyeifungia Prisons mabao 10 msimu uliomalizika, amesema anatambua changamoto iliyo mbele yake baada ya kusajiliwa na mabingwa hao wa Tanzania Bara msimu huu, lakini amesema atajituma kuhakikisha anaingia kwenye kikosi cha kwanza cha Simba.
Mbali na Rashid, Simba imekamilisha usajili wa washambuliaji Adam Salamba kutoka Lipuli FC na Marcel Kaheza kutoka Majimaji.
Timu hiyo sasa itakuwa na washambuliaji watano ukiongeza na wawili waliokuwepo Emanuel Okwi na John Bocco.
Simba pia inakusudia kusajili mshambuliaji mmoja wa Kimataifa.
Simba huenda ikaachana na Laudirt Mavugo, Juma Liuzio ambao mikataba yao imemalizika

ADVERTISE HERE