Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo Jumatano limepanga ratiba ya Kombe la FA (Azam Sports Federation) ambalo Mabingwa watetezi ni Simba.
TFF limepanga jumla ya timu 91 ambazo zitachuana kutoka timu za Mabingwa wa Mikoa, Daraja la Pili (SDL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na ligi kuu.
Mechi za kwanza za Kombe hilo zinatarajiwa kupigwa kuanzia Oktoba 31 mwaka huu hadi Novemba 2.
Michezo ya kwanza itazikutanisha timu za Buseresere (Geita) dhidi ya Green (Songwe), Kisarawe United (Pwani) itacheza na Silabu (Mtwara) na Usamala (Simiyu) wao watapambana na Sahare All Stars (Tanga).
Upangaji huo wa ratiba ulisimamiwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi.
Mchanganuo wa timu hizo ni: 16 za Ligi Kuu, 24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL); 24 za Ligi Daraja la Pili (SDL) na 27 za Ligi ya Mabingwa wa Mkoa (RCL).

ADVERTISE HERE