Hatma ya Kichuya kujulikana akitoka Nairobi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Jun 2018
Hatma ya Kichuya kujulikana akitoka Nairobi
Kiungo mshambuliaji Shiza Kichuya pamoja na kikosi cha wachezaji 18 wa Simba wapo Nairobi kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup inayotarajiwa kuanza keshokutwa Juni 03.

Hata hivyo mkataba wa Kichuya wa kuitumikia Simba unamalizika mwezi huu na winga huyo bado hajasaini mkataba mpya.

Kumekuwa na taarifa kuwa Kichuya amekuwa akiwindwa na vilabu vya Azam FC na Yanga wakati baba yake amemtaka asubiri ofa kutoka klabu ya TP Mazembe iliyoonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Kichuya amekataa kuzungumzia hatma yake katika klabu ya Simba hadi atakaporejea kutoka nchini Kenya.

"Suala la usajili litajulikana tu, kwa sasa akili yangu na hata wachezaji wenzangu tunaielekeza Nairobi kwenye michuano ya Sportpesa lengo tunataka ubingwa," alisema Kichuya jana kabla hajasafiri na kikosi cha Simba kwenda Nairobi.

Uongozi wa Simba umedhamiria kumbakisha kwa gharama yoyote kiungo huyo aliyen'gara katika kikosi cha Simba msimu huu
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’