Simba ilivyosomba wakali wote wa mabao VPL

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
1 Jun 2018
Simba ilivyosomba wakali wote wa mabao VPL
Kama wapinzani wa Simba katika Ligi Kuu Bara wanadhani mabingwa hao wameridhika na taji la msimu huu, pole yao na wanapaswa kujipanga kwelikweli.

Hii ni kwa sababu Simba ndio kwanza inatengeneza kikosi kikali kama wembe baada ya kukusanya kijiji kilichobeba jumla ya mabao 73.

Ndio, Simba imeshawasajili Marcel Kaheza kutoka Majimaji na Adam Salamba wa Lipuli huku ikiendelea kumalizana na Mohammed Rashid wa Prisons, ambao wanaungana na Emmanuel Okwi, John Bocco na Shiza Kichuya waliopo Msimbazi.

Sasa ukichukua mabao yaliyofungwa na wachezaji hao wanaotarajiwa kuanza kuvaa uzi wenye rangi nyekundu na nyeupe, sambamba na wanaowakuta kikosini, Simba ina kikosi cha mabao 73.

Kaheza amemaliza msimu akiwa na mabao 14 kama Bocco wakati Mo Rashid alifunga 10 na Salamba alitupia kambani mabao manane, jumla ya mabao hayo ni 32.

Lakini katika msimu huu nyota watatu wa Msimbazi, Okwi, Bocco na Kichuya utatu wao uilitengeneza mabao 41 kati ya 62 yaliyofungwa na timu hiyo kwa msimu mzima.

Ukiyachukua mabao ya watatu hao na yale ya akina Kaheza unatengeneza jumla ya mabao 73, hivyo kuwapa kazi timu pinzani kuhakikisha zinafanya usajili wa maana wa mabeki la sivyo zitaumia kwani safu hiyo ya Simba itakata kama wembe.

Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre ndiye aliyependekeza usajili huo wa aina yake akivutiwa na nguvu za Salamba mwenye akili ya kufunga kama alivyowafanya mabeki wake katika sare ya bao 1-1. Salamba alifunga bao akimburuza beki Yusuf Mlipili.

Ukiachana na Salamba ambaye tayari sasa ameanza maisha mapya akiwa na gari ya kisasa aina ya Toyota Crown kama anayoitumia Okwi, Kaheza ambaye aliwahi kulelewa na Simba naye tayari ameshamwaga wino wa miaka miwili akirudi katika klabu yake ya zamani naye kama alivyokuwa Salamba amefunga mabao 14 msimu uliomalizika akitakiwa kuyaleta mabao hayo kwa Wekundu hao.

Marcel katika mabao hayo bao moja maridadi la kisigino aliwafunga Simba wenyewe katika mchezo wa mwisho wa ligi

Hawakuishia hapo Simba wanaposema sajilini mabeki wanamaanisha kwani wametua tena kwa straika mwingine Mo Rashid wa Prisons katika msimu huu amemaliza kwa kutupia wavuni jumla ya mabao 10.

Inaelezwa Simba wanakaribia kumalizana na mshambuliaji huyo wakiwa tayari wameshamaliza mazungumzo ya awali wanachosubiri ni kukubaliana ada ya uhamisho na mambo ya kusaini.

Kocha Lechantre alisema mapema usajili wake ulikuwa unataka kuwa na safu kali ambayo itaweza kuifunga timu yoyote akilenga zaidi michuano ya kimataifa, kwani hakufurahishwa na hali ilivyokuwa kwa Simba kuwategemea zaidi Okwi na Bocco tu.

“Nataka wachezaji wanaoweza kufunga kama Okwi na Bocco, ili hawa wakikosekana, basi wanaokuwepo waifanye kazi hiyo kwa ufanisi,” alisema Mfaransa huyo.

Mmoja wa vigogo wa usajili wa Simba amesema kuwa zoezi la usajili linaendelea kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi kwani baada ya kumaliza safu ya mbele itafuata eneo la kati, mabeki na kuongeza kipa, huku akificha majina ya nyota wanaowanyemelea kwa sasa.

“Subirini tu, wenyewe mtaiona kazi inayoendelea Msimbazi,” alisema kigogo huyo.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
43m ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →