Tathmin ya Julio kuelekea mpambano wa watani wa Jadi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
25 Oct 2017
Tathmin ya Julio kuelekea mpambano wa watani wa Jadi
Kocha wa Dodoma FC ya Mkoani Dodoma, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameitaka timu yake ya zamani ya Simba kuwa makini na mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu, Jumamosi katika mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga.

Jumamosi kuna mchezo wa Simba na Yanga na mashabiki wamekuwa wakiusubiri kwa hamu kubwa kuona ni timu gani inaweza kuibuka na ushindi.

Julio ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba na kocha wa timu hiyo amesema kuwa Simba wanatakiwa kumlinda sana mshambuliaji huyo kwa kuwa sasa amebadilika siyo kama zamani.

Julio alisema, mchezo huo unatarajia kuwa mgumu na wenye upinzani wa hali ya juu na kuwataka Simba wasiibeze Yanga kwa kuwa ina kikosi kizuri na wanacheza mpira wa kueleweka.

“Ajibu ni mchezaji mzuri ana kiwango cha hali ya juu sio yule aliyekuwa Simba, hivyo ni mchezaji wa kuchungwa sana katika mchezo huo, naamini mchezo huo utakuwa mgumu na wenye upinzani wa hali ya juu.

“Simba wanahitaji kuwa makini na siyo kama nasema vibaya ila naamini kutakuwa na ushindani mkubwa katika mechi hiyo ijapokuwa naamini mechi itakuwa na ugumu wa hali ya juu kutokana na kila upande kujiandaa ipasavyo.

“Mechi hii mara nyingi huwa inakuwa haina mwenyewe kutokana na kila upande kujiandaa vyema kuelekea mchezo huu hivyo tunasubiria siku ya Jumamosi,” alisema Julio.

CHAMPIONI
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE →