Kaheza aahidi makubwa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 May 2018
Kaheza aahidi makubwa Simba
Baada ya kusaini mkataba mpya wa kurejea Simba, mshambuliaji, Marcel Kaheza, ameahidi kuisaidia timu yake kufanya vizuri zaidi katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa itakayoshiriki.

Kabla ya kwenda Majimaji, Kaheza alikuwa ni mchezaji wa timu ya vijana ya umri chini ya miaka 20 maarufu Simba B.

Baada ya kurejea tena Simba, Kaheza amesema sasa ameiva na yuko tayari kupambana kuisadia Simba iweze kufanya vema kutokana na kupata uzoefu.

Kaheza amesmea ameshakuwa mzoefu na anaifahamu vema Ligi Kuu Bara pamoja na changamoto zake tofauti na awali alivyokuwa Simba.

"Napenda kuwaahidi kuwa ninakuja Simba kivingine, nimekua na ninaweza kupambana, kipindi kile ilikuwa ni sababu ya umri na wachezaji waliokuwapo wakati ule, nawaahidi nitaisaidia kupata mafanikio zaidi," alisema mshambuliaji huyo.

Aliongeza kuwa anaweza kuitumikia klabu hiyo katika mazingira yoyote kwa sababu anaamini changamoto katika soka la Afrika ni jambo la kawaida.

Mbali na Kaheza, wachezaji wengine wapya waliosajiliwa na Simba ni pamoja na Adam Salamba kutoka Lipuli ya Iringa na Mohamed Rashid wa Tanzania Prisons ya jijini Mbeya.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’