Simba kupeleka 'full mziki' Kenya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 May 2018
Simba kupeleka 'full mziki' Kenya
Baada ya kukamilika kwa msimu wa ligi kuu ya Vodacom jana, kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka keshokutwa Alhamisi May 31 kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup.

Uongozi wa Simba umesema utapeleka nchini Kenya kikosi kamili kilichotwaa ubingwa wa VPL msimu huu pamoja na wachezaji wapya wanaotarajiwa kuitumikia timu hiyo msimu ujao.

Tayari SportPesa imetoa ratiba ya michuano hiyo itakayoendeshwa kwa mfumo wa mtoano.

Siku ya ufunguzi Juni 03, saa saba kamili mchana, Yanga itachuana na KK HomeBoyz kwenye mchezo wa ufunguzi.

Baadae siku hiyo hiyo Gor Mahia itachuana na JKU mchezo ukitarajiwa kuanza saa tisa na robo wakati Simba wao watacheza Juni 04 dhidi ya K Sharks saa tisa kamili Alasiri.

Singida United ambayo Juni 02 inakabiliwa na mchezo wa fainali ya kombe la FA dhidi ya Mtibwa Sugar, itashuka dimbani Juni 05 kucheza na AFC Leopards mchezo ukitarajiwa kuanza saa tisa Alasiri.

Timu nne zitakazoshinda michezo ya kwanza zitatinga hatua ya nusu fainali.

Michezo ya nusu fainali itapigwa Juni 07 wakati ile ya fainali na mshindi wa tatu na nne itapigwa Juni 10.

Bingwa wa michuano hiyo atajinyakulia karibu Mil 68 pamoja na kupata nafasi ya kusafiri kwenda nchini Uingereza kucheza na Everton inayoshiriki Premie Ligi mchezo ukipigwa katika dimba la Goodison Park
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
34m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’