Baada ya Salamba na Kaheza nani aje?

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 May 2018
Baada ya Salamba na Kaheza nani aje?
Wakati ligi kuu ikimalizika jana, uongozi wa Simba tayari umekamilisha usajili wa wachezaji wawili 'waliotesa' katika msimu huo.

Marcel Kaheza mshambuliaji wa Majimaji ndiye aliyekuwa wa kwanza kusaini mkataba wa miaka miaka miwili Msimbazi.

Jana Kaheza aliifunga bao timu yake hiyo mpya kwenye mchezo wa kufunga msimu uliomalizika kwa sare ya bao 1-1. Bao la Simba lilifungwa na Haruna Niyonzima.

Baada ya kumalizana na Kaheza, Simba ikahamia kwa mshambuliaji Adam Salamba aliyekuwa ametakiwa kwa mkopo na klabu ya Yanga kutoka Lipuli FC.

Salamba amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Simba.

Baada ya kuwapata washambuliaji hao wazawa, Simba inasubiri sahihi ya mshambuliaji mmoja wa Kimataifa, mkongwe Chris Katongo.

Simba imedhamiria kuimarisha kikosi chake tayari kwa msimu ujao pamoja na ligi ya mabingwa inayoanza mwezi Disemba.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
12h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’