Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom msimu huu Simba, leo wanashuka kwenye uwanja wa Majimaji kuwakabili wenyeji wao kwenye mchezo wa mwisho wa kukamilisha msimu.
Mchezo huo ni wa kukamilisha ratiba kwa Simba lakini una umuhimu wa kipekee kwa Majimaji inayohitaji kushinda ili iweze kubaki ligi kuu.
Majimaji yenye alama 24 ni lazima iifunge Simba na wakati huo huo ikiomba Ndanda FC ifungwe na Stand United.
Kama Ndanda itapata sare dhidi ya Stand, Majimaji italazimika kuifunga Simba zaidi ya mabao matatu.
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema mabingwa hao wa Tanzania hawawezi kutumika kama ngazi, na watahakikisha wanaondoka na alama zote tatu.
TFF imetahadharisha kwa timu zisijaribu kupanga matokeo kwenye michezo ya leo ya kukamilisha msimu.

ADVERTISE HERE