Manara amuwakia 'Julio' na wapinga mabadiliko wengine

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 May 2018
Manara amuwakia 'Julio' na wapinga mabadiliko wengine
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Simba Haji Manara amewataka wanachama wa klabu hiyo wanaopinga mabadiliko kuacha tabia hiyo ya usaliti.

Manara amemtaka kocha na mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo 'Julio' pamoja na wanachama wengine wanaopinga mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji yaliyopitishwa kuwa ni " wasaliti' kwa sababu walitakiwa kufika na kutoa maoni yao kwenye mkutano na si mahali kwingine.

Kama kuna mwanachama awe maarufu, asiwe maarufu, alipaswa aje katika kikao cha Mei 20, kukaa na kuzungumza mitandaoni kutafuta umaarufu, ...lakini inapokuja suala la Simba Sports Club, na ukaivuruga kwa dhamira yako chafu, sitakuacha, sitajali heshima yako, sitajali umri wako, kwa maslahi machafu kuja kutuchafua, nitapambana na yoyote anayezuia mabadiliko," alisema Manara.

Msemaji huyo alilazimika kumjibu Julio, baada ya kusambaa kwa sauti ya kocha huyo ikipinga uamuzi uliopitishwa wa kuendesha klabu hiyo kwa mfumo wa hisa huku akimkataa mfanyabiashara bilionea, Mohamed Dewji 'Mo' ambaye ameridhia kununua hisa asilimia 49 kwa dau la bilioni 20.

Simba tayari imefanya marekebisho ya Katiba yake na sasa tayari imeanza mchakato wa kubadili mfumo wake wa uendeshaji.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’