Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wameondoka leo kwenda Songea, Ruvuma wakiwa na kikosi imara na kilichokamilika ili kuwavaa wenyeji Majimaji katika mechi ya mwisho ya ligi hiyo itakayofanyika Jumatatu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Majimaji mjini humo.
"Timu itaondoka Jumamosi alfajiri, tunaenda tukiwa 'full mzuka', ni mechi muhimu kama zilivyokuwa mechi nyingine zilizopita," alisema Manara jana.
Mbio zilizobakia katika ligi hiyo ni kwa upande wa timu zinazopambana kuepuka janga la kushuka daraja, kwa sasa tayari Njombe Mji imeshashuka na inachosubiriwa ni timu itakayoungana nao kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.
Majimaji inahitaji kupata ushindi dhidi ya Simba ili iweze kubaki ligi kuu huku ikiiombea mabaya Ndanda FC kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Stand United.

ADVERTISE HERE