Simba yashauriwa isake wasaidizi wa Bocco, Okwi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
26 May 2018
Simba yashauriwa isake wasaidizi wa Bocco, Okwi
Winga wa zamani wa Simba, Mnenge Suluja amekiangalia kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, kisha akatamka maneno mazito.

Amesema Simba haiwezi kupambana kama hakutaletwa mastraika matata ili kuwa mbadala wa washambuliaji Emmanuel Okwi na John Bocco, ambao wamekinukisha kinoma msimu huu.

Suluja amesema ameifuatilia Simba kwa makini kwenye mechi zake za Ligi Kuu na amegundua pacha hao wanapokesana kikosi basi huwa ni majanga na timu inapwaya.

Kwenye mahojiano na Mwanaspoti jana, Suluja alisema usajili ujao wa Simba, mabosi wanapaswwa kutuliza akili na kusajili washambuliaji makini na wanaojua kupasia nyavuni ili kuipa makali zaidi timu yake hiyo.

Alisema Okwi na Bocco wakikosekana timu hiyo inakuwa inayumba kwa kuwa, hakuna mbadala jambo ambalo limeonekana wazi katika mechi ambazo nyota hao wawili hawapo.

“Unaona pale kwenye ushambuliaji akikosekana Bocco au Okwi basi timu inakuwa haiko sawa katika kufunga, sasa inatakiwa wasajili washambuliaji mbadala ambao ni wazoefu na wanaolijua goli,” alisema Suluja.

Hata hivyo, winga huyo aliwapongeza nyota wa Simba kwa kuweza kunyakuwa ubingwa huo na amesema kilichobaki sasa wajipange kwa ajili ya michuano mikubwa ya Afrika na watashiriki katika Klabu Bingwa Afrika mwakani.

“Kwanza niwapongeze kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, kazi bado haijaisha wanatakiwa sasa kujiandaa mapema kwa mashindano ya kimataifa ili nako wafanye vyema,” aliongeza.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →