Simba 'yafagilia' udhamini wa SportPesa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 May 2018
Simba 'yafagilia' udhamini wa SportPesa
Uongozi wa klabu ya Simba umekiri kuwa udhamini madhubuti wanaoupata kutoka kwa kampuni ya Sportpesa pamoja na kujituma kwa wachezaji ndio siri ya ubingwa wao wa ligi kuu Tanzania Bara walioutwaa msimu huu.

Kufuatia kutwaa ubingwa huo, Kampuni ya Sportpesa jana iliwakabidhi hundi ya Shilingi milioni 100 kama makubaliano yao ya mkataba yanavyoeleza.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa hundi hiyo, Makamu wa Rais wa Simba, Iddi Kajuna, alisema kuwa kuendesha klabu ya soka ni kazi kubwa na gharama lakini ujio wa kampuni hiyo ya kubashiri michezo kuliwaondolea ugumu huo.

"Hakuna kitu kigumu kama kulipa mishahara kwa wachezaji na wafanyakazi wengine wa klabu na uendeshwaji mzima wa timu, tangu tumekuwa na Sportpesa mambo yameenda vizuri kutokana na udhamini wao," alisema Kajuna.

"Wamekuwa wakikamilisha mahitaji ya kimkataba mapema na kutufanya kuweza kulipa mishahara mapema kati ya tarehe 26 na 28," aliongezea kusema.

Alisema baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu, sasa wanajipanga kuhakikisha wanatwaa kombe la Sportpesa Super Cup kabla ya kuanza kushiriki michuano ya Afrika inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

"Tutaenda na kikosi kamili Nairobi kwa ajili ya michuano hii, lengo ni kutwaa ubingwa na kupata nafasi ya kwenda England kucheza na Everton, tunaamini wachezaji wetu watatwaa ubingwa na kupata nafasi ya kujitangaza zaidi, lakini pia ni kuanza kufanyia kazi kauli ya Rais wetu Magufuli ya kutaka tupambane kuchukua makombe makubwa ya Afrika," alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Sportpesa, Abbas Tarimba, alisema wanajivunia kuona Simba wanaowadhamini wamefanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu.

"Kama makubaliano yetu ya mkataba yanayotaka, leo (jana) tunatimiza ahadi yetu kwa kuwakabidhi hundi yao, tunaamini hata kwenye michuano ya Sportpesa Super Cup Simba wataiwakilisha vyema nchi na kutwaa ubingwa," alisema Tarimba.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Pavel Slavkov ambaye naye aliwapongeza wachezaji pamoja na viongozi wa timu hiyo kwa ubingwa.

Katika hatua nyingine, Simba inaondoka kesho kwenda Songea kwa ajili ya mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu dhidi ya Majimaji utakaochezwa Jumatatu kwenye uwanja wa Majimaji.

Baada ya mchezo huo, Simba itaanza safari ya kuelekea Nairobi kwa ajili ya michuano hiyo ya Sportpesa inayotarajiwa kuanza Juni 3 na kumalizika Juni 10.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’