Njombe Mji imekuwa timu ya kwanza kuteremka daraja baada ya Ndanda kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa leo katika dimba la Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Ushindi wa leo umeifanya Ndanda ifikishe alama 26 na kuchupa hadi nafasi ya 14 hivyo kuiporomosha ligi daraja la kwanza Njombe Mji yenye alama 22.
Majimaji yenye alama 24 inaweza kuifuata Njombe Mji ligi daraja la kwanza kama itashindwa kuifunga Simba kwenye mchezo wa mwisho Jumatatu ijayo, May 28 2018 huku ikiiombea Ndanda FC ipoteze dhidi ya Stand United.
Njombe Mji yenyewe itakuwa inakamilisha ratiba tu kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mwadui FC

ADVERTISE HERE