Mayanga atangaza kikosi cha Stars kitakachoivaa Benin

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Oct 2017
Mayanga atangaza kikosi cha Stars kitakachoivaa Benin
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza kikosi c ha wachezaji 24, kitakachoingia kambini mwezi ujao kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin.

Taifa Stars itacheza mechi hiyo ya kirafiki ugenini Novemba 11, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kocha Mayanga achukue jukumu hilo.

Tanzania katika mchezo uliopita wa kirafiki dhidi ya Malawi ililazimisha sare ya bao 1-1 matokeo yaliyoiporomosha kwa nafasi 11 katika viwango vya Fifa hadi kufikika 136.

Wakati Tanzania ikiwa ya 136, katika viwango hivyo wapinzani wao Benin ipo nafasi ya 79 katika ubora wa Fifa na mwezi uliopita walipanda kwa nafasi tisa (9).

Katika kikosi hicho kocha Mayanga ameita wachezaji watatu wa kikosi cha timu ya vijana na wazoefu 21 tayari kwa mchezo huo.

Kikosi cha Stars kinaundwa na Makipa ni Aishi Manula(Simba), Ramadhani Kabwili (Yanga) na Peter Manyika (Singida United).

Mabeki ni Gadiel Michael (Yanga), Erasto Nyoni (Simba), Boniface Maganga (Mbao FC), Nurdin Chona(Tanzania Prisons), Abdi Banda (Baroka FC, Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Yanga) na Dickson Job (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Himid Mao (Azam), Hamis Abdallah (Sonny Sugar, Kenya), Mzamiru Yassin (Simba), Raphael Daud (Yanga),Simon Msuva (Difaa El Jadidi, Morocco), Shiza Kichuya (Simba), Farid Mussa (Tenerife, Hispania), Abdul Hilal (Tusker, Kenya), Mohammed Issa (Mtibwa Sugar) na Ibrahim Ajib (Yanga).

Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Mbaraka Yusuph (Azam), Elias Maguri (Dhofar, Oman) na Yohana Mkomola (Etoile du Sahel, Tunisia).
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
21m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
18h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
21h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE β†’