Wachezaji 30 kuwania tuzo ya mchezaji bora wa VPL

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 May 2018
Wachezaji 30 kuwania tuzo ya mchezaji bora wa VPL
Jumla ya wachezaji 30 wameteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa VPL msimu wa 2017/18.

Sherehe za utoaji wa tuzo msimu huu zitafanyika Juni 23 ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.

Afisa Habari wa TFF Clifford Ndimbo amewaambia waandishi wa Habari leo kuwa mwaka huu kumekuwa na marekebisho ambapo amesema baadhi ya tuzo zimeondolewa na nyingine kuongezwa.

Ndimbo amesema TFF imefuta tuzo ya Mchezaji Bora wa Kigeni, ambayo mwaka jana ilichukuliwa na kiungo Mzimbabwe wa Yanga, Thabani Kamusiko.

Lakini kumeongezwa tuzo ya Mwamuzi Bora Msaidizi ambayo haikuwepo msimu uliopita.

Tuzo zitakazotolewa ni Bingwa, Mshindi wa Pili, Mshindi wa Tatu, Mshindi wa Nne, Mfungaji Bora, Timu yenye nidhamu, Mchezaji Bora chini ya umri wa miaka 20, aambayo imepewa jina la Tuzo ya Ismail Khalfan, Mchezaji Bora Chipukizi, Mwamuzi Bora Msaidizi, Mwamuzi Bora, Kipa Bora, Kocha Bora, Bao Bora Kikosi Bora cha Wachezaji 11 wa Ligi Kuu na Mchezaji wa Heshima.

Orodha ya awali ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya mchezaji bora ni;

Habibu Kyombo (Mbao FC), Khamis Mcha (Ruvu Shooting FC), Yahya Zayed (Azam FC), Razack Abalora (Azam FC), Bruce Kangwa (Azam FC), Aggrey Morris (Azam FC), Himid Mao (Azam FC), Awesu Awesu (Mwadui FC), Adam Salamba (Lipuli FC), Mohammed Rashid (Prisons FC), Shafiq Batambuze (Singida United) na Mudathir Yahya wa Singida United.
Wengine ni Marcel Kaheza wa Maji Maji FC, Ditram Nchimbi wa Njombe Mji FC, Eliud Ambokile wa Mbeya City, Shaaban Nditi, Hassan Dilunga wote wa wa Mtibwa Sugar, Tafadzwa Kutinyu wa Singida United, Ibrahim Ajib, Gardiel Michael, Papy Tshishimbi, Kelvin Yondani, Obrey Chirwa wote wa Yanga SC, Aishi Manula, Emmanuel Okwi, John Bocco, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Shiza Kichuya na Asante Kwasi wote kutoka Simba

Tuzo ya mchezaji bora wa VPL msimu uliopita ilichukuliwa na beki wa kushoto wa Simba Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr'

Mwaka kutakuwa na michuyo mitatu ambapo orodha ya kwanza itachujwa na kubaki 10 watakaoingia katika awamu ya pili ya mchujo itakayobakisha wachezaji watatu.

Katika hao watatu mmoja ndiye ataibuka na tuzo ya mchezaji bora wa msimu
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
29m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’