Mbeya City nayo yawa kampuni, kukusanya mtaji wa Bil 100

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 May 2018
Mbeya City nayo yawa kampuni, kukusanya mtaji wa Bil 100
Klabu ya Mbeya City imekuwa klabu ya pili kubadili mfumo wake wa uendeshaji na kuwa kampuni, baada ya Simba kufanya hivyo.

Jana Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Emmanuel Kimbe katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari alisema kampuni hiyo imesajiliwa Januari 26, mwaka huu na Msajili wa Makampuni na Biashara (BRELA) chini ya sheria ya makampuni ya mwaka 2002, inaitwa Mbeya City Football Club Public Limited Company (Mbeya City FC PLC) kwa hati namba 140785 na imesajiliwa pia na Posta Mbeya kwa anuani namba 663.

Kimbe amesema kwamba Mbeya City FC PLC inatarajia kukusanya mtaji wa Shilingi Bilioni 100 ili kujiendesha kwa ufanisi.

Katika mfumo huo, Halmashauri ambaye ni mmiliki ataamua ni sehemu gani (asilimia) ya hisa atakazobaki nazo na nyingine zitapelekwa kwenye soko la mitaji ili kutafuta wamiliki/wabia wengine. Hisa hizo zitakuwa wazi kwa watu wote waliopo ndani na nje ya nchi.

Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni na Menejimenti ya timu itaundwa upya baada ya wanahisa wote kupatikana
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
33m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’