Baada ya kuiwezesha Simba kutwaa ubingwa msimu huu, kocha Mkuu wa mabingwa hao Pierre Lechantre tayari ameanza mikakati kwa ajili ya msimu ujao.
Lechantre aliyependa masihara, amesema msimu ujao ataongeza ukali kwa wachezaji watakaokwenda kinyuma na taratibu zake.
Akizungumza nasi juzi, Lechantre amesema katika kikosi chake sasa hakutakuwa na nafasi kwa wachezaji wavivu, wasio wakweli na wazembe.
Amesema kwa kuwa Simba itashiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, ni lazima kuwa na kikosi imara chenye wachezaji wanaofahamu vyema wajibu wao.
Kocha huyo mwenye uraia wa Ufaransa anakusudia kuanza mapema maandalizi ya kikosi cha Simba akianza na masuala ya usajili muda mfupi baada ya kumalizika mchezo dhidi ya Majimaji Jumatatu ijayo.

ADVERTISE HERE