Tayari msimu umemalizika, May 28 ndiyo siku ya mwisho kabisa ya msimu wa 2017/18 ambapo Simba wameshakabidhiwa ubingwa.
Zoezi la usajili kwa ajili ya msimu ujao limeanza ingawa sio rasmi hadi pale dirisha litakapofunguliwa rasmi wiki chache zijazo.
Shiza Kichuya, mmoja wa viungo mahiri walioiwezesha Simba kutwaa ubingwa mkataba wake wa kuwatumikia mabingwa hao unamalizika mwezi ujao.
Baba mzazi wa kiungo huyo Ramadhani Kichuya amemzuia mwanawe asiharakishe kusaini mkataba mpya mpaka pale atakapofahamu hatma yake na klabu ya TP Mazembe.
Kiwango alichoonyesha Kichuya msimu huu kimezivutia timu nyingi huku TP Mazembe ikielezwa kuwa tayari kumsajili mchezaji huyo.
Hata hivyo taarifa za uhakika ni kwamba Bosi wa Simba Mohammed Dewji 'Mo' anataka kumbakisha Kichuya Msimbazi.
Simba imedhamiria kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

ADVERTISE HERE