Nahodha John Bocco, Aishi Manula, Shomari Kapombe na Erasto Nyoni walisajiliwa na klabu ya Simba wote wakitoka Azam FC baada ya kumaliza mikataba yao.
Baada ya klabu ya Azam FC kutangaza kuweka kikomo cha pesa za usajili pamoja na kupunguza mishahara ya wachezaji wake, wanne hao walioamua kuondoka na kusajiliwa na Simba.
Hakika uongozi wa Simba uliramba dume kwani hakuna shaka wababe hao wamechangia kwa kiasi kikubwa ubingwa wa VPL kwenda Msimbazi.
Bocco ameingia Simba na moja kwa moja akateuliwa kuwa nahodha na kocha wa awali Joseph Omog ambaye aliwahi kufanya nae kazi msimu wa 2013/14 katika klabu ya Azam FC.
Bila shaka Manula ataibuka mlinda lango bora msimu huu na utakuwa ni msimu wa pili mfululizo kushinda tuzo hiyo aliyoishinda akiwa na Azam FC msimu uliopita.
Manula hajafungwa kwenye michezo 18 kati ya 28 aliyokaa langoni katika kikosi cha Simba
Hakuna shaka Bocco, Erasto Nyoni na Shomari Kapombe nao wataingia katika kikosi bora cha VPL msimu huu.

ADVERTISE HERE