Okwi aomba radhi mashabiki Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 May 2018
Okwi aomba radhi mashabiki Simba
Katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar juzi, Emanuel Okwi mshambuliaji kinara wa mabao kwenye kikosi cha Simba alikosa mkwaju muhimu wa penati kwenye dakika za majeruhi na kuwafanya mabingwa hao wapoteze mchezo katika siku waliyokabidhiwa taji na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk John Magufuli.

Okwi amewaomba radhi mashabiki wa Simba kwa tukio hilo ambalo amekiri halitafutika katika kumbukumbu zake.

Mazingira ya tukio hilo ndiyo yaliyomfanya Okwi ajisikie vibaya.

Simba ilikuwa haijapoteza mchezo kwenye ligi hivyo ingekuwa fahari na kumbukumbu nzuri kumaliza msimu bila ya kufungwa.

Lakini siku hiyo pia ilikuwa kama siku ya sherehe kwa klabu ya Simba, hakuna aliyependa kuiona Simba inafungwa kwenye siku yake muhimu.

"Tumeumia kama wachezaji, haikuwa lengo letu na hasa mimi kitendo cha kukosa penalti ambayo ingebadilisha matokeo, tutajitahidi kuhakikisha mchezo ujao ambao utakuwa wa mwisho tunamaliza vizuri," amesema Okwi.

Kipa mkongwe wa Kagera Sugar Juma Kaseja ambaye aliidakia kwa mafanikio makubwa klabu ya Simba, ndiye aliyeharibu sherehe baada ya kudaka mkwaju wa Okwi

Simba itasafiri mkoani Ruvuma kumaliza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Majimaji.

Mchezo huo sasa hautakuwa na maana yoyote kwa Simba baada ya kuharibu rekodi yake ya kutofungwa msimu huu lakini utakuwa na umuhimu mkubwa kwa Majimaji ambayo inajinusuru na hatari ya kuteremka daraja
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’