Azam FC yaipiku Yanga nafasi ya pili

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 May 2018
Azam FC yaipiku Yanga nafasi ya pili
Ushindi wa mabao 4-1 iliyopata Azam FC jana dhidi ya Prisons umeiweka kwenye mazingira mazuri ya kumaliza nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu ya Vodacom.

Ushindi huo umeifanya Azam FC ifikishe alama 55 ikiwa ni alama saba zaidi ya Yanga yenye michezo miwili ya kiporo.

Hata kama Yanga itashinda michezo yake miwili itafikisha alama 54 na italazimika kushinda mchezo wa mwisho baina ya timu hizo ili kuweza kumaliza nafasi ya pili

Aidha mshambuliaji wa Azam FC Shabani Iddi aliyefunga mabao matatu 'hat-trik' kwenye mchezo huo sasa amefikisha mabao nane msimu huu.

Baada ya Simba kutwaa ubingwa mapema vita kubwa iliyobaki ni baina ya timu zinazojaribu kujinusuru na kuteremka daraja.

Njombe Mji, Ndanda FC na Majimaji zinatofautiana kwa alama mbili pekee huku Njombe Mji iliyochapwa bao 1-0 na Mtibwa jana ikiwa mkiani na alama 22.

Ndanda FC yenye alama 23 ina mchezo mmoja wa kiporo dhidi ya Mwadui FC wakati Majimaji ina alama 24 na mchezo wa mwisho inamaliza dhidi ya mabingwa, Simba.

Kama Ndanda itashinda dhidi ya Mwadui May 23 basi Njombe Mji itakuwa timu ya kwanza kuteremka daraja.

Lakini matokeo yakiwa tofauti timu zote tatu zitakuwa na nafasi ya kujitetea kwenye michezo yao ya mwisho ambayo itafanyika katika viwanja vyao vya nyumbani.

May 28 Ndanda itacheza na Stand United, Njombe Mji itacheza na Mwadui FC wakati Majimaji itacheza na Simba.

Timu mbili zitashuka daraja msimu huu wakati timu sita tayari zimepanda kutoka ligi daraja la kwanza.

Jumla ya timu 20 zitashiriki ligi kuu ya Vodacom msimu ujao.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’