Katika Mkutano Mkuu wa dharura wa klabu ya Simba uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam, uongozi wa Simba umemzawadia jezi yenye namba 19 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh John Pombe Magufuli.
Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' alimkabidhi jezi hiyo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe.
Try Again amesema kuwa zawadi hiyo ilipaswa kutolewa jana lakini kutokana na ufinyu wa muda, zoezi hilo lilishindwa kufanyika.
Waziri Mwakyembe aliyealikwa kwenye Mkutano huo kwa niaba ya Serikali, amebariki mabadiliko ya katiba Simba ambayo yanaenda kuupokea rasmi mfumo mpya na wa kisasa wa uendeshwaji wa klabu hiyo.
Dk Mwakyembe amesema ni wakati mwafaka sasa kwa klabu za Tanzania kuingia katika mfumo huu ambao umejikita kibiashara na wenye mafanikio makubwa huku akieleza kuwa haukwepeki.
Aidha Mwakyembe amempongeza Mfanyabiashara Mohammed Dewji 'Mo' kwa kuamua kuwekeza ndani ya Simba akiamini ataibadilisha zaidi klabu hiyo kuweza kufika mbali kimataifa.
Baada ya kueleza hayo, Mwakyembe amesema serikali imeruhusu rasmi mabadiliko hayo kwa kuzingatia Mwekezaji lazima awekeze kwa asilimia 49 na wanachama wasalie na 51.

ADVERTISE HERE