Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk John Pombe Magufuli leo ameikabidhi simba ubingwa wa VPL baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar.
Hata hivyo Kagera Sugar imetibua sherehe ya ubingwa kwa mabingw hao wapya baada ya kuondoka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Edward Christofer katika mchezo ambao Emanuel Okwi alishindwa kuisawazishia Simba kwenye dakika za majeruhi baada ya kukosa mkwaju wa penati.
Rais Magufuli ameipongeza Simba kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kusubiri kwa misimu mitano.
Pia amezipongeza timu nyingine zilizoshiriki ligi msimu huu.
Rais Magufuli alimkabidhi kombe nahodha wa Simba John Bocco na kuamsha vifijo na nderemo kwenye uwanja wa Taifa uliofurika maelfu ya mashabiki wa Simba.

ADVERTISE HERE