Lechantre avutiwa na watano Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
18 May 2018
Lechantre avutiwa na watano Simba
Mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Simba wamefanya usajili wa nyota 12 katika dirisha kubwa na nyota mmoja Asante Kwasi kutoka Lipuli katika dirisha dogo, lakini ni watano tu waliomkosha kocha Mfaransa, Pierre Lechantre.

Lechantre alisema katika kikosi chake tangu ametua hapa nchini miezi mitano iliyopita, amebaini kuwa usajili mkubwa uliofanywa na uongozi ulikuwa mzuri kuliko timu yoyote hapa nchini.

Kocha huyo aliyewahi kumnoa mchezaji bora mara nne Afrika, Samuel Et’oo, alisema alikuta timu ipo katika hali nzuri na wachezaji wazuri ila kulikuwa na vitu vidogo ambavyo aliviongezea na timu kuweza kuimarika zaidi.

Wachezaji ambao wamemkosha zaidi Mfaransa huyo ni Shomary Kapombe, Aishi Manula, Emmanuel Okwi, John Bocco na Erasto Nyoni na kuweka wazi kuwa, wamekuwa na msaada kufanikisha timu kubeba ubingwa, lakini wasingeweza kufanya hivyo bila kushirikiana na wenzao.

“Wachezaji wote wapo vizuri lakini kwa hao wanastahili pongezi kwa kila mmoja kwa nafasi yake alivyocheza pia yupo Jonas Mkude alikuwa vizuri ingawa muda mwingine alikuwa ananikera. Ana uvivu fulani,” alisema.

“Nimefundisha soka nchini nyingi na kwa viwango vya Kapombe, Manula, Mkude, Bocco, Okwi na Nyoni wanaweza kucheza soka hata Ufaransa.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
12h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →