Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Simba Haji Manara amewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kesho mapema kwenye uwanja wa Taifa tayari kwa sherehe za ubingwa zinazotarajia kuanza mapema sana.
Mchezo wa Simba dhidi ya Kagera Sugar unatarajia kuanza saa 8:15 mchana na baada ya kumalizika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk John Magufuli atawakabidhi kombe la ubingwa wa VPL msimu huu, Simba wababe ambao hawajapoteza mchezo msimu huu.
Manara amewataka mashabiki kujitokeza mapema uwanja wa Taifa kwani mageti yatafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi.
Kampuni ya Selcom tayari imeanza kuuza tiketi za kuweza kushuhudia yatakayojiri katika siku hiyo maalumu na ya kihistria kwa klabu ya Simba.
Baada ya kupunguzwa, kiingilio cha Mzunguuko sasa ni Tsh 2,000/- wakati VIP A ni Tsh 15,000/- na VIP B ni Tsh 10,000/-
Pia tiketi zitaendelea kuuzwa uwanjani.

ADVERTISE HERE