Baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar kupangwa kuchezwa saa nane mchana, kikosi cha Simba leo kimeanza kujifua mchana ili kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo.
Kocha Mkuu wa Simba Pierre Lechantre anaongoza mazoezi ya vijana wake katika viwanja vya Hotel ya White Sands jijini Dar es salaam.
Simba itacheza na Kagera Sugar keshokutwa Jumamosi, May 19 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 29, mchezo utakaopigwa katika dimba la uwanja wa Taifa na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli.
Baada ya mchezo huo Rais Magufuli atawakabidhi kombe mabingwa hao wapya wa VPL sambamba na kupokea kombe la CECAFA kutoka kwa vijana wa Serengeti Boyz waliloshinda Burundi hivi karibuni.

ADVERTISE HERE