Ndoto ya Simba ya kuwa klabu tajiri Afrika Mashariki inatarajia kukamilika baada ya mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed ‘Mo’ Dewji kuridhia kiasi cha umiliki wa hisa katika klabu hiyo, ambao utapitishwa kwenye mkutano mkuu utakaofanyika Jumapili kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere DSM.
Dewji ameridhia kumiliki asilimia 49 na wanachama watabaki na asilimia 51 ya hisa za klabu hiyo baada ya kufuata maelekezo yaliyotolewa na serikali.
Awali, mfanyabiashara na mdhamini huyo wa zamani wa mabingwa hao, aliomba kumiliki hisa asilimia 50 za klabu hiyo na kiasi kingine kitabakia kwa wanachama.
Awali Mo, aliridhia kuwekeza kiasi cha Sh. bilioni 20 kupata hisa kwa asilimia 51, hivyo kwa mantiki hiyo sasa atawekeza dau hilo kwa kununua hisa 49, hivyo kuifanya Simba kuanza mabadiliko ya kuelekea kuwa miongoni mwa klabu zinazoendeshwa kisasa duniani.
Akizungumza jana jijini, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema wanachama wa klabu hiyo hawatakiwi kupoteza fursa hiyo muhimu ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu yao katika mkutano utakaofanyika Jumapili.
Manara alisema ili klabu iweze kujiendesha kisasa na kushindana na klabu nyingine kubwa zilizoendelea Afrika, katika kusajili wachezaji wenye ubora na kutwaa mataji makubwa, wakati wa kubadili mfumo umefika na wanachama wanatakiwa kutokubali kurudi nyuma.
"Tunawashukuru SportPesa wametusitiri, Simba sio kisiwa, tukikosa kutumia fursa hii, tutakuwa kama wenzetu tunaowacheka...tulishawahi kukaa miezi minne bila ya mishahara, tuliwahi kuzuiwa basi letu Shinyanga kwa sababu ya deni la milioni tatu,...hatuwezi kwenda na mfumo huu, hatuwezi kwenda na katiba hizi, hatuwezi kuwa na timu ya Taifa bora kwa mfumo huu, " alisema Manara

ADVERTISE HERE