Simba inarekebisha Katiba ili iendeshwe kisasa - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 May 2018
Simba inarekebisha Katiba ili iendeshwe kisasa - Manara
Kwenye Mkutano wake na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya SImba Haji Manara ametoa ufafanuzi kwa nini klabu hiyo inakwenda kurekebisha Katiba yake Jumapili ijayo.

Manara amesema kuwa Simba inaenda kufanya mabadiliko ya Katiba yatakayoifanya Simba iendeshwe katika mfumo kwa kisasa zaidi.

Manara ameeleza kuwa Simba ina zaidi ya miaka 82 mpaka sasa lakini imekuwa ikiendeshwa kwa kutegemea ada za wanachama ambazo hazijitoshelezi kuleta manufaa ndani ya klabu.

Ameongeza kuwa licha ya ada za wanachama, Simba imekuwa ikitegemea zaidi mashabiki Uwanjani ili kupata mapato yatakayoweza kuendesha timu kwa ujumla haswa na ulipaji wa fedha za wachezaji au mishahara.

Katika mkutano Mkuu utakaofanyika Jumapili ya wiki hii, Simba inaenda kuzungumzia rasmi muundo wa kisasa wa klabu ili kujiendesha kibiashara zaidi tofauti na kuendelea kutegemea wanachama.

Simba itawapa nafasi wanachama kumiliki hisa zao huku ikiwatengenezea Kampuni yao itakayojulikana kwa jina la Simba Sports Club Company Holding Limited ambayo itakuwa chini ya Baraza la Wadhamini wa klabu.

Vilevile klabu hiyo itaweza kubadilika jina kutoka Simba Sports Club mpaka Simba Sports Club Company Limited kwa lengo la kujiendesha zaidi kibiashara.

Manara amewaomba wanachama kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo Jumapili ya wiki hii ili kuweza kuweka historia kubwa ya soka la Tanzania, Afrika Mashariki kwa Ujumla na Kati haswa kwenye soka.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’