Rais Magufuli aombwa aikabidhi Simba ubingwa wa VPL 2017/18

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 May 2018
Rais Magufuli aombwa aikabidhi Simba ubingwa wa VPL 2017/18
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. John Pombe Joseph Magufuli, ameombwa awe mgeni rasmi katika mchezo Simba SC dhidi ya Kagera Sugar FC utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mei 19 2018.

Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia, amesema kuwa wamemwandikia barua Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dokta Harrison Mwakyembe yenye ombi la kumuhitaji Magufuli juu ya ugeni huo.

Karia ameeleza kuwa Rais Magufuli atapata wasaa wa kukabidhi kombe la 19 mabingwa wapya wa Ligi Kuu msimu huu wa 2017/18 ambalo wamelipata wakiwa hawajapoteza mchezo wowote msimu huu.

Mbali na Simba kukabidhiwa taji hilo katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Magufuli atawakabidhi pia vijana wa Serengeti Boys Kombe la CEFACA chini ya miaka 17 walilolitwaa nchini Burundi baada ya kuifunga Somalia kwa mabao 2-0 kwenye mechi ya fainali iliyopigwa Uwanja wa Ngozi, jijini Bujumbura.

Sherehe za Simba na Serengeti Boys zitaanza majira ya saa 8 mchana huku viiingilio vya mchezo huo (Simba SC vs Kagera Sugar) vikiwa ni 15,000 kwa VIP A, 7000 kwa VIP B na C pia 3000 kwa sehemu ya mzunguko.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’