Wakili ajitoa kumtetea Hanspoppe

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 May 2018
Wakili ajitoa kumtetea Hanspoppe
Jana Wakili Lugona Mwakipesile alijitokeza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi, kumtetea Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba, Zacharia Hanspoppe.

Mwakipesile anayemtetea Hanspoppe aliyeunganishwa katika kesi ya utakatishaji fedha na kugushi inayowakabili vigogo wa klabu hiyo, alilazimika kujiondoa katika kesi hiyo, baada ya upande wa mashtaka kumtaka amlete mshtakiwa mahakamani.

Hanspoppe na Mfanyabiashara, Franklin Lauwo waliunganishwa katika kesi inayowakabili Rais wa Simba Evance Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu', katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. April 30, 2018, mahakama hiyo iliamuru washtakiwa Hanspoppe na Lauwo wakamatwe popote walipo.

Mahakama ilitoa amri hiyo baada ya upande wa mashtaka kupitia kwa Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Leonard Swai kuieleza kuwa wamewatafuta washtakiwa hao tangu Machi 16 mwaka huu bila mafanikio.

Lakini jana Wakili Mwakipesile alifika mahakamani hapo na kuieleleza mahakama kuwa amefika kumwakilisha Hanspoppe, ambaye yupo nje ya nchi.

Itakumbukwa kuwa, Aprili 30, mwaka huu Mahakama ya Kisutu, ilitoa amri kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba, Zacharia Hanspoppe na mwenzake ambaye ni Mfanyabiashara, Franklin Lauwo wakamatwe popote walipo.

Awali, Swai alidai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa Aveva bado ni mgonjwa ana ameshindwa kufika mahakamani huku mwenzake , Kaburu akiwepo mahakamani hapo.

Baada ya kupitia hoja za pande zote, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 28, mwaka huu ambapo atatoa uamuzi kama mahakama hiyo inauwezo wa kuondoa mshtakiwa wa tatu na wanne katika kesi hiyo au laa

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka kumi likiwemo la kula njama, matumizi mabaya na kughushi nyaraka ikionyesha Simba inalipa mkopo wa USD 300,000 kwa Aveva kitu ambacho sio kweli.

Pia wanadaiwa Machi 10 na 16, 2016, Aveva na Nyange waliandaa nyaraka za kuhamisha dola za kimarekani 3000,000 kutoka kwenye akaunti ya klabu ya simba kwenda kwenye akaunti ya Aveva wakijua kuwa wanachofanya ni kosa.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’