Mabingwa mara 19 wa Ligi Kuu Bara kikosi cha Simba, leo Jumatatu wameliteka Bunge la Tanzania jijini Dodoma baada ya kutua katika ofisi hizo.
Mabingwa hao wa msimu huu wameongozwa na wachezaji, benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi na muda huu wapo Bungeni baada ya kupata mwaliko wa Spika Job Ndugai.
Hata kabla hawajatambulishwa na Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga, lakini Naibu Waziri wa Tamisemi, Joseph Kakunda ndiye ameanzishwa 'shangwe' bungeni humo.
Kakunda kabla ya kujibu swali Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), Almas Maige, Naibu Waziri huyo ameanza kwa kusema, leo Mei 14, 2018 ameamka saa 10 alfajili kujiandaa kujibu maswali lakini kubwa ni furaha ya ubingwa.
Huku wabunge wakishangilia, Kakunda akiwa mwenye furaha amesema: "Sasa naamini Watanzania watapata wawakilishi wazuri wa michuano ya kimataifa, hawatatupa presha."
Hakuwa Kakunda pakee, bali hata Mbunge wa Ilala (CCM), Azzan Zungu amesimama na kuuliza swali la kutaka kujua mikakati ya kuboresha michezo kwa vijana amesema.
"Humu ndani kaingia mnyama mkali sana, lakini tuko salama," amesema Zungu na shangwe kuendelea ukumbini.
Kakunda ambaye muda wote amekuwa akijibu maswali, amekuwa akichombeza maneno ya furaha ya ubingwa huo ikiwamo kuungana na Zungu amesema, anaungana nae kwenye furaha yake ambayo anaijua.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE