Simba yaanza mkakati wa kumbakisha Kichuya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 May 2018
Simba yaanza mkakati wa kumbakisha Kichuya
Sio jambo la kushangaza kuona timu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi zinapigana vikumbo kumuwania kiungo mshambuliaji wa simba, Shiza Kichuya.

Kiwango alichoonyesha Kichuya msimu huu kimemfanya awe na thamani kubwa na yenye manufaa kwake kama mchezaji.

Kichuya ndiye kinara wa kutengeneza mabao kwenye ligi kuu ya Vodacom akiwa amepika mabao 20 na mwenyewe kufunga saba.

Mkataba wake wa kuitumikia Simba unamalizika mwishoni mwa mwezi huu ambapo Wakala wake amesema mteja wake hayuko tayari kuanza mazungumzo ya mkataba mpya kabla wa awali haujamalizika.

Lakini taarifa za uhakika tayari mabosi wa Simba wameanza jitihada za kumbakisha kiungo huyo ambaye anahitajika sana kwenye kikosi cha Simba ambacho mwakani kitashiriki michuano ya ligi ya mabingwa.

Bilionea wa Simba, Mo Dewji ambaye atakabidhiwa timu siku chache zijazo ameapa kumbakisha mchezaji huyo kwa gharama yoyote.

Kuna taarifa kuwa Azam FC na Yanga zinamuwania Kichuya baada ya kubaini bado hajasaini mkataba mpya.

TP Mazembe ilikuwa ya kwanza kutuma ofa ya kumtaka ambayo ilikataliwa mapema na uongozi wa Simba huku vilabu kadhaa kutoka Misri na Afrika Kusini navyo vikiunga tela.

Mshambuliaji wa Everton Yanick Balasie ambaye alikuja nchini wakati timu ya Taifa ya DR Congo ilipokuja kucheza mchezo wa kirafiki na Tanzania, alimtabiria Kichuya kuwa kwa kiwango chake anaweza kusajiliwa na timu yoyote barani Ulaya.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’